Mwongozo wa faragha wa Google Payments kwa watoto
Chagua umri wako: Miaka 6 hadi 8 Miaka 9 hadi 12
Umri wa miaka 6 hadi 8
Ungependa kujua jinsi Google inavyolinda taarifa zako za Google Payments?
Ukurasa huu unawalenga watoto! Unajibu maswali kama vile jinsi Google inavyotumia taarifa zako kwenye Google Payments na kuzilinda.
Kwa wazazi: Maelezo haya yanatumika tu kwenye Akaunti za Google zinazosimamiwa kupitia Family Link, kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi uliko). Ili upate maelezo zaidi, angalia Ilani yetu ya Faragha na Sera yetu ya Faragha.
Google inahitaji taarifa gani?
Kando na taarifa ambazo Google hukusanya kwa bidhaa zote, huwa tunahitaji pia baadhi ya taarifa za msingi kutoka kwako ili kufanya Google Payments ifanye kazi vizuri.
Taarifa za kujisajili
- Anwani na namba yako ya simu
- Siku yako ya kuzaliwa
- Taarifa kuhusu kadi yako ya mikopo au ya malipo
- Taarifa za kutumiwa kuthibitisha utambulisho wako
Wakati mwingine, tunaweza kuomba taarifa zaidi ili kusaidia kuangalia kama kila kitu kiko salama.
Taarifa kutoka sehemu nyingine
- Taarifa kuhusu malipo yako kwenye maduka
- Taarifa za benki na kadi yako ya mikopo au ya malipo
Taarifa za kila unaponunua kitu
- Ulinunua lini na wapi pamoja na bei yake
- Iwe ulitumia kadi ya mikopo au ya malipo
Google hutumia taarifa zangu kufanya nini?
Kando na jinsi Google inavyotumia taarifa zako kwa bidhaa zote, pia tunatumia taarifa unazotupatia kufanya mambo kwenye Google Payments kama vile:
- Kukurahisishia mchakato wa malipo
- Kukuonyesha pamoja na wazazi wako malipo uliyofanya
- Kumpa mzazi wako usaidizi ikiwa unauhitaji
- Kusaidia kulinda taarifa na pesa zako dhidi ya watu wabaya
- Kuhakikisha kuwa unafuata kanuni za Google Payments
- Kuamua ikiwa malipo utakayofanya baadaye ni salama
Je, Google huruhusu taarifa zangu zifikiwe na wengine?
Kando na njia ambazo Google huruhusu taarifa zako zifikiwe kwa bidhaa zote, tunaweza pia kuruhusu taarifa zako zifikiwe na wengine ili kufanya Google Payments ifanye kazi. Ifuatayo ni mifano michache:
- Ikiwa sheria inasema tunaweza
- Ili kusaidia kuhakikisha kuwa malipo na akaunti yako inafanya kazi na ni salama
- Ili kuhakikisha malipo unayofanya yanakamilika
Wazazi wangu wana udhibiti gani?
Yafuatayo ni mambo ambayo wazazi wako wanaweza kufanya:
- Kukuwekea kadi mpya kwenye Google Payments
- Kupata barua pepe unapotumia kadi zako na kadi inapoondolewa
- Kuangalia malipo unayofanya na kuondoa kadi za malipo katika Family Link
Google hulinda taarifa zangu vipi?
Google inajitahidi kusaidia kulinda taarifa zako. Unaweza kusaidia kwa kuweka siri PIN na manenosiri yako.
Mambo muhimu ya kukumbuka:
- Kuwa mwangalifu kuhusu unayemruhusu afikie akaunti yako.
- Kuwa mwangalifu ni nani unayemruhusu atumie kifaa chako.
- Ikiwa unafikiri Google Payments yako si salama tena, mwambie mzazi wako.
Umri wa miaka 9 hadi 12
Ungependa kujua kuhusu faragha yako unapotumia Google Payments?
Upo kunakofaa! Soma maswali yanayoulizwa sana na watoto, kama vile jinsi tunavyotumia taarifa zako na kusaidia kuzilinda.
Wazazi, taarifa hii inatumika tu kwenye Akaunti za Google zinazosimamiwa kupitia Family Link, kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi uliko). Ili upate maelezo zaidi, angalia Ilani yetu ya Faragha na Sera yetu ya Faragha.
Google inahitaji taarifa gani?
Kando na taarifa ambazo Google hukusanya kwa bidhaa zote, huenda pia tukahitaji kuomba taarifa nyingine ili kuhakikisha kuwa Google Payments inakufaa.
Taarifa za kujisajili
Haya ni baadhi ya maelezo ambayo tutahifadhi kwenye Akaunti yako ya Google. Baadhi ya data inaweza kuhifadhiwa kwenye kifaa chako.
- Anwani
- Namba ya simu
- Tarehe ya kuzaliwa
- Taarifa za kadi ya mikopo au ya malipo
- Taarifa za kutumiwa kuthibitisha utambulisho wako, kama vile kitambulisho
Wakati mwingine, tunaweza kukuomba ututumie taarifa zaidi, au ujibu maswali ili kusaidia kuthibitisha taarifa au utambulisho wako.
Taarifa kutoka sehemu nyingine
Tunaweza kupata taarifa kukuhusu kutoka sehemu nyingine, kama vile:
- Maelezo kutoka kwenye miamala yako ya Google Payments katika maduka
- Maelezo kuhusu jinsi unavyotumia njia zako za kulipa na akaunti kutoka sehemu nyingine zilizounganishwa na Google Payments
- Benki au kampuni iliyotoa kadi yako
- Manufaa kutokana na njia yako ya kulipa
- Taarifa kuhusu malipo yako kutoka sehemu nyingine, ili kusaidia kuhakikisha kuwa akaunti na malipo yako yanaaminika
Taarifa za kila unaponunua kitu
Unapotumia Google Payments kununua kitu, tunaweza kukusanya taarifa kuhusu muamala huo, kama vile:
- Tarehe, saa na kiasi
- Maelezo na mahali duka lilipo
- Njia uliyotumia kulipa
Google hutumia taarifa zangu kufanya nini?
Kando na jinsi Google inavyotumia taarifa zako kwa bidhaa zote, tunatumia maelezo unayotuma kufanya mambo kama vile:
- Kumwezesha mtu amsaidie mzazi wako iwapo kuna matatizo kwenye Google Payments yako (kama vile huduma kwa wateja)
- Kusaidia kuimarisha usalama wako, wa wengine na wa taarifa za Google dhidi ya watu wanaoweza kujaribu kuchukua taarifa zako au kutumia pesa zako bila ruhusa yako
- Kusaidia maduka au kampuni nyingine kukupa ulichoomba
- Kuhakikisha unafuata kanuni za Google Payments
- Kufanya uamuzi kuhusu miamala yako ya baadaye kwenye Google Payments
- Kuhakikisha unajua kuhusu manufaa mengine ya njia yako ya kulipa
Tunaweza kuhifadhi taarifa unazotupatia kwa muda wote unaotumia Google Payments na labda hata zaidi ikiwa tunahitaji kufuata sheria.
Je, Google huruhusu taarifa zangu zifikiwe kila mara?
Kando na jinsi Google huruhusu taarifa zako zifikiwe kwa bidhaa zote, kuna sababu nyingine chache tu zinazoweza kutufanya turuhusu zifikiwe na watu wengine nje ya Google, kama vile:
- Ikiwa sheria inaturuhusu
- Ili akaunti yako iendelee kutumika, kuhakikisha kuwa ununuzi wako unafanyika, kuimarisha usalama wa akaunti yako, kukulinda dhidi ya mtu anayejaribu kukuibia au kukudanganya au kwa madhumuni ya shughuli zetu za kila siku
- Ili kusaidia kuhakikisha kuwa njia yako ya kulipa ni salama na bado inafanya kazi
- Ili ukamilishe usajili ulioomba wa huduma inayotolewa na washirika wengine
Google inamiliki au inadhibiti baadhi ya kampuni nyingine. Wakati mwingine tunaruhusu zifikie taarifa zako ikiwa zinazihitaji ili zitekeleze shughuli za kila siku. Hiyo inajumuisha taarifa yoyote tunayoweza kupata kutoka sehemu nyingine, kama vile maduka unamonunua.
Wazazi wangu wana udhibiti gani?
Hivi ndivyo mzazi wako anaweza kufanya
- Kutoa idhini ana kwa ana kwa kila kadi ya malipo inayowekwa
- Kupata barua pepe unapotumia kadi zako na kadi inapoondolewa
- Kukagua miamala yako ya Google Payments na kuondoa kadi za malipo kwenye Family Link
Google Pay hulinda taarifa zangu vipi?
Google inafanya mambo mengi ili kukulinda, lakini ni muhimu uweke siri PIN, manenosiri ya akaunti yako pamoja na taarifa nyingine muhimu.
Kumbuka:
- Ukiruhusu taarifa za Akaunti yako ya Google zifikiwe na washirika wengine, wataweza kufikia taarifa zako za malipo kwenye Google pamoja na taarifa zako binafsi
- Kuwa mwangalifu na unayemruhusu afikie kifaa chako au programu yako ya Pochi ya Google
Ikiwa unafikiri programu yako ya Pochi ya Google si salama tena, mwombe mzazi wako msaada ili aweze kuijulisha Google.
Mara ya mwisho kusasishwa: Tarehe 16 Machi, 2026
© 2026 Google – Google Sheria na Masharti ya Google Ilani za Faragha Zilizotangulia