Ilani ya Faragha ya Google Payments

Ilibadilishwa mwisho tarehe 8 Septemba 2019

Sera ya Faragha ya Google inafafanua jinsi tunavyoshughulikia taarifa binafsi unapotumia bidhaa na huduma za Google. Huduma ya Google Payments inatolewa kwa wamiliki wa Akaunti za Google na inatumika kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Google. Ilani hii ya Faragha pia inaeleza kuhusu desturi za faragha za Google zinazotumika kwenye Google Payments.

Unapotumia Google Payments, unatakiwa kuzingatia Sheria na Masharti ya Google Payments ambayo yanaeleza kwa kina zaidi kuhusu Huduma zilizojumuishwa katika Ilani hii ya Faragha. Maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo hayajafafanuliwa katika Ilani hii ya Faragha ya Google Payments yanafasiliwa katika Sheria na Masharti ya Google Payments.

Ilani ya Faragha ya Google Payments inatumika katika Huduma zinazotolewa na kampuni zinazomilikiwa kikamilifu na Google LLC, ikijumuisha Google Payment Corp. ('GPC'). Tafadhali soma Sheria na Masharti ya Google Payments yanayopatikana katika Huduma ili upate maelezo kuhusu kampuni inayomilikiwa na Google, inayotoa Huduma husika. Ikiwa wewe ni mtumiaji (isipokuwa wanaouza kwenye soko la Google) unayeishi nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, kidhibiti cha data kwa ajili ya taarifa yako ni Google Ireland Limited. Ikiwa wewe ni mtumiaji katika nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, bila kujumuisha Uingereza na unauza kwenye soko la Google, kidhibiti cha data kwa ajili ya taarifa yako ni Google Payment Ireland Limited. ikiwa unaishi Uingereza na unauza kwenye soko la Google, kidhibiti cha data kwa ajili ya taarifa yako ni Google Payment Limited.

Maelezo tunayokusanya

Kando na maelezo yaliyoorodheshwa katika Sera ya Faragha ya Google, tunaweza pia kukusanya maelezo yafuatayo:

Jinsi tunavyotumia maelezo tunayokusanya

Mbali na matumizi yaliyoorodheshwa katika Sera ya Faragha ya Google, tunatumia maelezo unayotupa na unayotoa kwa GPC, au kampuni zingine tunazomiliki na pia watu au kampuni nyingine, kukupa huduma tunazotoa kwa wateja wa Google Payments na kulinda haki, mali au usalama kwenye Google, watumiaji wetu, au umma, ikiwemo kukulinda dhidi ya ulaghai, wizi wa data ya binafsi au ukiukaji mwingine. Huenda maelezo kama haya yakatumika kusaidia washirika wengine kukupa huduma unazohitaji. Pia tunatumia maelezo haya kukagua Akaunti yako ya Google Payments ili kubaini ikiwa unatimiza sheria na masharti ya akaunti, kufanya maamuzi kuhusu miamala yako ya baadaye kwenye Google Payments na kwa ajili ya mahitaji mengine halali ya kibiashara yanayohusiana na miamala unayotekeleza kwenye Google Payments.

Unapojisajili, maelezo yako huhifadhiwa katika Akaunti yako ya Google na usajili wa njia yako ya kulipa huhifadhiwa kwenye seva za Google. Aidha, huenda baadhi ya vipengele vya data vikahifadhiwa kwenye kifaa chako cha mkononi. Kwa lengo la kutii mchakato wa kisheria masharti ya udhibiti, tunaweza kuhifadhi maelezo unayotupatia kwa muda mrefu.

Maelezo tunayoshiriki

Tutashiriki tu taarifa yako binafsi na kampuni au watu wengine binafsi nje ya Google katika hali zifuatazo:

Kwa mfano, unapofanya ununuzi au kutekeleza muamala fulani ukitumia Google Payments, tutaruhusu taarifa fulani ya binafsi ifikiwe na kampuni au mtu binafsi unayenunua kwake au kufanya naye biashara. Hii inajumuisha kushiriki taarifa yako binafsi na msanidi programu uliyenunua kwake ukitumia Google Payments kwenye Google Play. Huenda pia ikajumuisha kutuma msimbo wako wa eneo au posta kwa tovuti au programu ya muuzaji unapotekeleza muamala ukitumia kitufe cha "Nunua ukitumia Google Pay" au kingine kama hicho, ili muuzaji aweze kuhesabu kodi na gharama za usafirishaji kwa ununuzi wako. Ukiongeza njia ya kulipa ya kampuni nyingine kwenye Akaunti yako ya Google Payments, tunaweza kumtumia mtoa huduma za malipo ya kampuni hiyo nyingine taarifa fulani binafsi, kama vile jina lako, picha ya wasifu, anwani ya barua pepe, anwani ya IP na ya kutuma bili, nambari ya simu, maelezo ya kifaa, mahali na maelezo ya shughuli ya Akaunti ya Google ikihitajika, ili kutoa huduma husika.

Unapotembelea programu au tovuti ya muuzaji husika, muuzaji huyo anaweza kuangalia iwapo una akaunti ya Google Payments yenye njia ya kulipa unayoweza kutumia kumlipa. Hii inasaidia kuchuja vipengele visivyotumika visionekane kwenye tovuti au programu.

Maelezo yoyote unayotoa moja kwa moja kwa muuzaji, tovuti au programu nyingine hayajumuishwi katika ilani hii ya faragha. Hatuwajibikii desturi za faragha au usalama za wauzaji au kampuni nyingine unazoshiriki nazo taarifa yako binafsi moja kwa moja. Tunakuhimiza ukague sera za faragha za watu au kampuni nyingine unazoshiriki nazo taarifa yako binafsi moja kwa moja.

Maelezo tunayokusanya, yakiwemo maelezo tunayopata kutoka kwa watu au kampuni nyingine, hushirikiwa na washirika wetu, yaani kampuni zinazomilikiwa na kudhibitiwa na Google LLC. Washirika wetu, ambao wanaweza kuwa taasisi za kifedha na zisizo za kifedha, hutumia maelezo haya kwa madhumuni yao ya kawaida ya kibiashara.

Una haki ya kujiondoa kwenye hali fulani ya kushiriki maelezo kati ya GPC na washirika wake. Hasa, unaweza kujiondoa katika:

Pia unaweza kujiondoa kwenye huduma ya Google LLC au washirika wake, ya kushiriki na muuzaji mwingine, unayetembelea tovuti au programu yake, kuwa una akaunti ya Google Payments unayoweza kutumia kumlipa muuzaji huyo.

Ukijiondoa, chaguo lako litatekelezwa hadi utakapobadilisha.

Ikiwa hungependa tushiriki taarifa binafsi kuhusu ustahiki wako wa kupokea mikopo kati ya GPC na washirika wake, au ikiwa hutaki washirika wetu watumie taarifa yako binafsi tuliyokusanya na kushiriki nao kwa madhumuni ya biashara, au ikiwa hutaki Google LLC au washirika wake kumjulisha muuzaji mwingine, unayetembelea tovuti au programu yake, kuwa una akaunti ya Google Payments unayoweza kutumia kumlipa muuzaji huyo, tafadhali weka mapendeleo kwa kuingia katika akaunti yako, kisha uende kwenye ukurasa wa mipangilio ya faragha ya Google Payments ili kusasisha mapendeleo yako.

Hatutashiriki taarifa yako binafsi na mtu yeyote aliye nje ya GPC au na washirika wetu isipokuwa katika hali iliyobainishwa kwenye ilani hii ya faragha. Kama ilivyoelezwa hapa juu, Google Payments ni bidhaa inayotolewa kwa wamiliki wa Akaunti za Google. Data unayotoa kwa Google LLC kwa madhumuni ya kufungua Akaunti ya Google, haiathiriwi na masharti ya kujiondoa yaliyotajwa kwenye ilani hii.

Usalama wa maelezo

Kwa maelezo zaidi kuhusu desturi yetu ya usalama, tafadhali soma Sera ya Faragha ya Google.

Usalama wa Akaunti yako ya Google Payments unategemea jinsi utakavyoweka kwa usiri nenosiri au manenosiri ya akaunti, PIN na vitambulisho vingine vya Huduma hii. Ukishiriki maelezo ya akaunti yako na mtu mwingine, atapata idhini ya kufikia akaunti na taarifa yako binafsi.

Ni wajibu wako kudhibiti ufikiaji wa kifaa chako cha mkononi na programu ya Google Payments kwenye kifaa chako, ikiwemo kutofichua nenosiri au manenosiri na/au PIN yako na kutoishiriki na yeyote. Pia ni wajibu wako kufahamisha Google au mshirika husika ikiwa unaamini kwamba usalama wa maelezo yaliyo katika programu ya Google Payments umeathiriwa.

© 2019 Google – Ukurasa wa Mwanzo wa Google Sheria na Masharti ya Google Ilani za Awali za Faragha