Ilani ya Faragha ya Google Payments

Ilisasishwa mara ya mwisho tarehe 23 Septemba, 2018

Sera ya Faragha ya Google inaeleza jinsi tunavyotumia maelezo ya binafsi unapotumia bidhaa na huduma za Google. Huduma ya Google Payments inatolewa kwa wamiliki wa Akaunti za Google na ni sharti utii Sera ya Faragha ya Google unapotumia huduma hii. Ilani hii ya Faragha pia inaelezea kuhusu desturi za faragha za Google ambazo ni mahususi kwa Google Payments.

Unapotumia Google Payments, unatakiwa kuzingatia Sheria na Masharti ya Google Payments ambayo yanaeleza kwa kina zaidi kuhusu Huduma zilizojumuishwa katika Ilani hii ya Faragha. Maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo hayajafafanuliwa katika Ilani hii ya Faragha ya Google Payments yanafasiliwa katika Sheria na Masharti ya Google Payments.

Ilani ya Faragha ya Google Payments inatumika katika Huduma zinazotolewa na kampuni zinazomilikiwa kikamilifu na Google LLC, ikijumuisha Google Payment Corp. ("GPC"). Tafadhali soma Sheria na Masharti ya Google Payments yanayopatikana katika Huduma ili upate maelezo kuhusu kampuni inayomilikiwa na Google, inayotoa Huduma husika.

Maelezo tunayokusanya

Kando na maelezo yaliyoorodheshwa katika Sera ya Faragha ya Google, huenda pia tukakusanya maelezo yafuatayo:

Jinsi tunavyotumia maelezo tunayokusanya

Mbali na matumizi yaliyoorodheshwa katika Sera ya Faragha ya Google, tunatumia maelezo unayotupa na unayotoa kwa GPC, au kampuni zingine tunazomiliki na pia kampuni zingine, ili tukupe huduma za Google Payments kwa ajili ya wateja na tukulinde dhidi ya ulaghai, wizi wa data ya binafsi au matumizi mabaya. Huenda maelezo kama haya yakatumika kusaidia kampuni zingine zikupe huduma au bidhaa unazohitaji. Pia tunatumia maelezo haya kukagua akaunti yako ya malipo ya Google ili tuthibitishe iwapo unaendelea kutimiza sheria na masharti ya akaunti hii, kufanya maamuzi kuhusu malipo ya baadaye katika Google Payments na kwa ajili ya mahitaji mengine halali ya kibiashara yanayohusiana na shughuli za malipo za Google Payments unazoanzisha.

Unapojisajili, maelezo yako huhifadhiwa katika Akaunti yako ya Google na usajili wa njia yako ya kulipa huhifadhiwa kwenye seva za Google. Aidha, huenda baadhi ya vipengele vya data vikahifadhiwa kwenye kifaa chako cha mkononi. Huenda tukahifadhi maelezo unayotupatia kwa muda mrefu kwa lengo la kutimiza mchakato na kanuni za kisheria.

Maelezo tunayoshiriki

Tutashiriki maelezo yako ya binafsi na kampuni zingine au watu binafsi nje ya Google katika hali zifuatazo:

Kwa mfano, unapofanya ununuzi au shughuli fulani ya kifedha ukitumia Google Payments, tutaruhusu maelezo fulani ya binafsi yapatikane kwa kampuni au mtu binafsi unayenunua kwake au kufanya naye biashara. Hii ni pamoja na kushiriki maelezo yako ya binafsi na msanidi programu ambaye ulinunua kwake ukitumia Google Payments katika Google Play. Ukiongeza aina ya malipo ya kampuni nyinginezo kwenye Akaunti yako ya Google Payments, tunaweza kumtumia mtoa huduma ya malipo wa kampuni nyingine maelezo fulani ya kibinafsi kukuhusu, kama vile jina lako, picha ya wasifu, anwani ya barua pepe, anwani ya IP na ya kutuma bili, nambari ya simu, maelezo ya kifaa, eneo na maelezo ya shughuli ya Akaunti ya Google ikihitajika ili kutoa huduma husika.

Unapotembelea programu au tovuti ya muuzaji husika, muuzaji huyo anaweza kuangalia iwapo una akaunti ya malipo ya Google yenye njia ya malipo unayoweza kuitumia kumlipa. Hii inakupunguzia uwezo wa kuona vipengele visivyotumika kwenye tovuti au programu.

Maelezo yoyote unayotoa moja kwa moja kwa muuzaji, tovuti au programu nyingine hayajumuishwi katika ilani hii ya faragha. Hatuwajibikii desturi za faragha au usalama wa wauzaji au kampuni zingine unazoshiriki nazo maelezo yako ya binafsi moja kwa moja. Tunakuhimiza ukague sera za faragha za watu au kampuni nyingine unazoshiriki nazo maelezo yako ya binafsi moja kwa moja.

Maelezo tunayokusanya, yakiwemo maelezo tunayopata kutoka kwa watu au kampuni nyingine, hushirikiwa na washirika wetu, yaani kampuni zinazomilikiwa na kudhibitiwa na Google LLC. Kampuni zetu nyingine zinaweza kuwa mashirika ya kifedha na yasiyo ya kifedha na yatatumia maelezo hayo kwa madhumuni ya shughuli zao za kawaida za kibiashara.

Una haki ya kujiondoa kwenye hali fulani ya kushiriki maelezo kati ya GPC na washirika wake. Hususan, unaweza kujiondoa kwenye:

Pia unaweza kuchagua kujiondoa ili Google LLC au washirika wake wasijulishe wauzaji wengine, ambao unatembelea tovuti au programu zao, kuwa una akaunti ya malipo ya Google ambayo inaweza kutumika kuwalipa wauzaji hao.

Ikiwa utachagua kujiondoa, chaguo lako litatekelezwa hadi utakapotushauri vinginevyo.

Ikiwa hutaki tushiriki maelezo ya binafsi kuhusu uwezo wako wa kupokea mikopo kati ya GPC na washirika wake; au ikiwa hutaki washirika wetu watumie maelezo yako ya binafsi tuliyokusanya na kushiriki nao kwa madhumuni ya mauzo; au ikiwa hutaki Google LLC au washirika wake kumjulisha muuzaji mwingine, ambaye unatembelea tovuti au programu yake, kuwa una akaunti ya malipo ya Google ambayo inaweza kutumika kumlipa muuzaji huyo, tafadhali weka mapendeleo yako kwa kuingia katika akaunti yako, uende kwenye ukurasa wa mipangilio ya faragha ya Google Payments na kusasisha mapendeleo yako.

Hatutashiriki maelezo yako ya binafsi na mtu yeyote aliye nje ya GPC au na washirika wetu isipokuwa katika hali iliyofafanuliwa katika ilani hii ya faragha. Kama ilivyoelezwa hapo juu, Google Payments ni bidhaa inayotolewa kwa wamiliki wa Akaunti ya Google. Data ambayo unatoa kwa Google LLC kwa madhumuni ya kujisajili kupata Akaunti ya Google, haiathiriwi na masharti ya kujiondoa kwenye ilani hii.

Usalama wa maelezo

Kwa maelezo zaidi kuhusu maadili yetu ya usalama, tafadhali angalia Sera ya Faragha ya Google.

Usalama wa akaunti yako ya malipo ya Google unategemea jinsi utakavyoweka nenosiri au manenosiri ya akaunti, PIN na maelezo mengine ya usiri wa Huduma hii. Ukishiriki maelezo ya akaunti yako na mtu mwingine, atapata uwezo wa kufikia akaunti na maelezo yako ya binafsi.

Ni wajibu wako kudhibiti uwezo wa kufikia kifaa chako cha mkononi na programu ya Google Payments kwenye kifaa chako, ikiwa ni pamoja na kulinda nenosiri au manenosiri na/au PIN yako na kutoishiriki na yeyote. Pia ni wajibu wako kufahamisha Google au mshirika husika ikiwa unaamini kwamba usalama wa maelezo yaliyo katika programu ya Google Payments umeathiriwa.

© 2018 Google - Ukurasa wa Kwanza wa Google Sheria na Masharti ya Google Ilani za Awali za Faragha